Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 2:24 am

NEWS: MAREKANI YATOA WARANTI KUKAMATWA KWA MELI YA IRAN GRACE 1

Wizara ya sheria ya marekani imetoa waranti jana Ijumaa (16.08.2019) ya kukamatwa kwa meli ya mafuta ya Iran Grace 1, siku moja baada ya jaji wa Gibraltar kuruhusu kuachiliwa kwa meli hiyo iliyokamatwa.

Wizara ya sheria inadai kuwa meli hiyo ni sehemu ya mpango "wa kufikia kinyume na sheria mfumo wa kifedha wa Marekani, kusaidia upelekaji kinyume na sheria mafuta nchini Syria kutoka Iran unaofanywa na jeshi la kulinda mapinduzi ya Kiislamu," ambayo Marekani imesema kuwa ni kundi la kigeni la kigaidi.

waranti huo unasema meli hiyo, ambayo bado imetia nanga katika eneo hilo linalo milikiwa na Uingereza la Gibraltar hadi jana Ijumaa, na mafuta yote yaliyomo katika meli hiyo yanalazimika kutaifishwa kwa misingi ya ukiukaji wa sheria ya kimataifa ya nguvu za dharura za kiuchumi , pamoja na kukamatwa kwa kiasi cha dola 995,000 , katika akaunti ambayo haikutajwa katika benki moja nchini Marekani inayoshrikiana na kampuni ya biashara ya Paradise Global Trading LLC, ambayo imeiita kampuni ya Shell inayohusishwa na biashara ambayo inafanyakazi kwa niaba ya jeshi la Iran.

Image result for Iran Grace 1

Hakuna taarifa za haraka kutoka Uingereza ama Gibraltar kuhusiana na iwapo watachukua hatua kuhusiana na waranti huo, wakati Iran imesema inatuma wafanyakazi wengine wapya kuiendesha meli hiyo pamoja na shehena yake xa mapipa milioni 2.1 ya mafuta.