- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAREKANI YAMTUMA KERRY KUWA MUANGALIZI WA UCHAGUZI KENYA
Washington: Nchi ya Marekani imemtuma aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa marekani John Kerry kuongoza jobo la waangaalizi wa uchaguzi mkuu wa Kenya unaopangwa kufanyika Agosti 8 mwaka huu.Ujumbe wa waangalizi 80 walioteuliwa na kituo cha Carter wakiongozwa na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry unatarajiwa kuwasili nchini Kenya wiki hii.
Kerry atafuatana na waangalizi wengine 80 ambao wametumwa na kituo cha Carter, Miongoni mwa waangalizi hao kutoka nchi 34 ni pamoja na aliyekuwa waziri mkuu wa Senegal, Amiata Toure.
Tangu Aprili mwaka huu waangalizi wamekuwa wakifuatilia matayarisho ya uchaguzi huo katika kaunti mbali mbali nchini Kenya.
Miezi miwili iliyopita rais wa Marekani Donald Trump aliteua kamati ya watu kumi kuongoza waangalizi watakaofuatilia uchaguzi mkuu wa Kenya.
“Ulimwengu mzima unasubiri kuona jinsi Kenya itakavyofanya uchaguzi wake Agosti”, alisema rais Trump alipokutana na wakuu wa bunge la Ulaya katika halfa iliyoandaliwa huko White-House.
Ripoti iliyotolewa wiki hii na kituo cha Carter iliisifu tume ya uchaguzi nchini Kenya kutokana na mikakati iliyoweka kusimamia uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti.
Kituo hicho pia kiliteuwa waangalizi kufuatilia uchaguzi mwingine uliofanyika mapema mwaka 2013, na kutoa ripoti iliyosema serikali ya Kenya ilijitahidi katika kuhakikisha uchaguzi ni wa kidemokrasia.
Lakini waangalizi hao walikosoa mirengo ya kisiasa iliyoongozwa na wanasiasa mashuhuri, rais Uhuru Kenyatta na kinara wa upinzani Raila Odinga.