- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAREKANI YAJIANDAA KUMUONDOA RAIS MADURO MADARAKANI
Marekani inapanga njia mbadala za kumshinikiza Rais Nicolas Maduro wa Venezuela kuachia madaraka pamoja na mikakati mingine ya kufikisha msaada kwa watu wa Venezuela katika taifa hilo liliharibika kiuchumi, baada ya juhudi za mwishoni mwa juma za kuingiza msaada kushindwa.
Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence leo Jumatatu anakwenda katika mji mkuu wa Colombia kukutana na wanachama wa muungano wa kikanda unaojulikana kama kundi la Lima, unaojumuisha nchi kadhaa za eneo hilo pamoja na kiongozi wa upinzani wa Venezuela, Juan Guaido, kujadiliana juu ya hatua zinazofuata zenye nia ya kumuondowa madarakani Maduro. Kwa mujibu wa afisa mmoja wa ngazi ya juu serikalini, Pence anatarajiwa kutangaza mipango ya wazi juu ya kuushughulikia mgogoro wa Venezuela.
Afisa huyo wa ngazi ya juu amewaambia waandishi habari kwamba watauonesha ulimwengu na Maduro kwamba Marekani inasimama pamoja na watu wa Venezuela pamoja na Guaido.