- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAREKANI YAIORODHESHA KAMPUNI YA HUAWEI TISHIO KWA USALAMA
Baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kutia saini amri ya kuizuwia makampuni ya Marekani kutumia vifaa vya mawasiliano vilivyotengenezwa na kile alichokieleza kuwa ni "mahasimu wa nje" (kampuni ya Huawei) ambao wanaelezwa kusababisha hatari ya usalama wa taifa, Katika hatua nyingine wizara ya biashara ya Marekani imeiongeza kampuni ya Huawei na mashirika yake katika orodha yake ya makampuni yanyoonekana kuwa ni kitisho kwa ama usalama wa taifa ama maslahi ya sera za mambo ya kigeni.
Amri hiyo inaelekea kuonesha wasi wasi wa Ikulu ya Marekani White House kwamba vifaa kutoka kwa wasambazaji wa China kama kampuni ya Huawei vinaweza kuleta kitisho katika mfumo wa mtandao wa Internet na mawasiliano.