Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 10:44 pm

NEWS: MAREKANI YAIONYA TANZANIA

Dar es Salaam. Ubalozi wa marekani kupitia Ofisa wake wa juu Bi Virginia Blaser amezungumzia wasiwasi wa marekani juu y viashiria vya uminywaji wa uwazi, haki za binadamu na utawala wa sheria na kusema visipo fanyiwa kazi mapema, vitaathiri biashara na maswala ya kiusalama katika nchi.

Blaser, ni ofisa wa juu wa Balozi Mdogo wa Marekani Afrika Mashariki, aliyazungumza hayo wakati akifanyiwa mahojiano maalumu na gazeti la The Citizen Alhamisi iliyopita, siku chache kabla ya kumaliza kipindi chake cha miaka minne.



Alisema wakati Serikali ikistahili pongezi kwa jitihada ilizoonyesha za kupambana na rushwa nchini, pia inatakiwa ichukue hatua kuendeleza uwazi na utawala wa sheria na kuangalia ishara zinazotia shaka ya kurudisha nyuma mambo, hasa sekta binafsi.

“Mustakabali wa Watanzania hauwezi kutegemea wadau wa maendeleo; hautatokana na ajira za serikalini; unatakiwa utoke katika sekta binafsi ambayo ni pana, imara, yenye hali nzuri na inayoaminika,” alisema.

“Na badala yake, naona ishara zinazokatisha tamaa katika sekta binafsi; na nina wasiwasi Tanzania itachukua njia gani.”

Aliongeza kuwa angependa kuona kampuni nyingi zaidi kutoka Marekani zikiingia nchini, lakini hilo litategemea zaidi “mazingira ya uwazi na yanayosaidia sekta binafsi