Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 10:28 am

NEWS: MAREKANI YAHARIBU MIFUMO YA KURUSHIA MAKOMBORA YA IRAN

Gazeti la Limeripoti kuwa Jeshi la Marekani limefanya mashambulizi ya udukuzi kwenye mifumo ya silaha za Irani.

Related image

Inaripotiwa kuwa Mashambulizi hayo ya mtandaoni yameharibu mifumo ya kompyuta inayodhibiti roketi na mitambo ya kurushia makombora ya nchi hiyo.

Hatua hiyo ya Marekani inakuja siku chache baada ya Rais wa Marekani Donald Trump alipoamua kuachana na mashambulizi ya anga dhidi ya nchi hiyo,

Tukio hilo linaonekana ni lakulipiza kisasi kwa tukio la kushambuliwa kwa ndege yake isiyo na rubani pia mashambulizi dhidi ya meli za mafuta ambazo Iran imedaiwa na Marekani kuziteketeza,New York Times imeeleza.

Related image

Mvutano kati ya Marekani na Iran ulijitokeza tangu Marekani ilipojiondoa kwenye mkataba wa nyukilia wa mwaka 2015 kati ya Iran na mataifa yenye nguvu duniani na kuiwekea vikwazo vilivyotikisa uchumi wa Iran.

Juma lililopita, Iran ilisema itaongeza viwango vilivyowekwa kwenye mkataba ule kuhusu mradi wa nyukilia.

Trump alisema hataki vita na Iran, lakini alionya kuwa Iran itakabiliwa na ''uharibifu'' ikiwa mzozo utatokea.

Mashambulizi yalipangwa kwa majuma kadhaa, vyanzo vimeviambia vyombo vya habari nchini Marekani ikaelezwa kuwa ni njia ya kulipa kisasi mashambulizi ya mabomu dhidi ya meli za mafuta kwenye Ghuba ya Oman.

Rais wa Marekani Donald Trump

Mashambulizi haya yamelenga mifumo ya silaha zinazotumiwa na majeshi ya nchi hiyo, yaliyoshambulia ndege isiyo na rubani ya rubani siku ya Alhamisi juma lililopita.

Kwa pamoja Washington Post na AP zimeeleza kuwa mashambulizi ya mtandao yameharibu mifumo.New York Times limesema ililenga kuzima mifumo hiyo kwa muda.