- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAREKANI YADHIBITISHA KUSHAMBULIWA NA MAKOMBORA YA IRAN
Wizara ya ulinzi ya Marekani imethibitisha kuwa Iran imezishambulia kwa makombora kambi zake mbili zilizoko Iraq ambazo zinawahifadhi wanajeshi wa Marekani na majeshi ya muungano yaliyoko nchini humo. Msemaji wa wizara hiyo, Jonathan Hoffman amesema ni wazi kwamba makombora hayo yamerushwa kutoka Iran.
Hoffman amesema kambi za kijeshi zilizoshambuliwa ziko Ain Assad na Erbil.
Televisheni ya taifa ya Iran imesema shambulizi hilo ni katika kulipa kisasi mauaji ya jenerali wa ngazi ya juu wa nchi hiyo, Qassem Soleimani aliyeuawa na Marekani. Hoffman amesema kambi hizo zimekuwa katika tahadhari ya juu kutokana na kuwepo dalili kwamba utawala wa Iran unapanga kuwashambulia wanajeshi wa Marekani na maslahi ya nchi hiyo katika eneo la Mashariki ya Kati.
Amesema Marekani itahakikisha inachukua hatua zote muhimu kuwalinda na kuwatetea raia na wafanyakazi wake pamoja na washirika wao katika ukanda huo.