- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAREKANI NA UINGEREZA WAMTETEA MWANDISHI ERICK KABENDERA
Dar es salaam: Nchi za Uingereza na Marekani kupitia Balozi zao nchini Tanzania wametoa tamko la pamoja wakionesha kusikitishwa kuhusu wasiwasi kwa kuzorota kwa haki za kisheria nchini Tanzania wakitolea mfano kitendo cha Serekali kupitia jeshi la Polisi kumshikilia mwandishi wa Habari za kiuchunguzi Erick kabendera
Katika tamko hilo, ofisi hizo mbili za ubalozi zinadai kuwa imedhihirika kwa zaidi ya mara moja watu kutiwa kizuizini kwa muda nchini Tanzania bila kupelekwa mahakamani na kubadilishiwa mashitaka na mamlaka zake za kisheria.
"Tuna wasiwasi hasa kwa tukio la hivi karibuni -- jinsi ambavyo halikushughulikiwa kwa haki la kukamatwa, kuwekwa kizuizini na tuhuma za mashtaka ya mwandishi wa habari za uchunguzi Bw Erick Kabendera, ikizingatiwa ukweli kwamba alinyimwa haki ya kuwa na mwanasheria kwenye hatua za awali na kutiwa kizuizini kwake, ambapo ni kinyume cha sheria ya makosa ya jinai," Limesema sehemu ya tamko hilo.
"Tunaisihi serikali ya Tanzania kutoa hakikisho la mchakato wa kutenda haki kisheria kwa raia wake, kama ilivyotambua kwamba ni haki ya msingi na kuridhia kwenye mikataba mbali mbali ya haki za kibinaadamu ya Umoja wa Mataifa, miongoni mwao ikiwemo azimio la kimataifa la haki za kirai na kisiasa."
Mwanahabari huyo meshtakiwa kwa makosa matatu ya ubadhirifu wa kiuchumi. Mosi anashtakiwa kwa kujihusisha na genge la uhalifu na uhujumu wa uchumi, pili kukwepa kulipa kodi ya zaidi ya milioni mia moja sabini za Kitanzania na tatu utakatishaji fedha zenye thamani ya zaidi ya millioni mia moja na sabini.
Erick Kabendera alipandishwa kizimbani Jumatatu ya wiki hii ikiwa ni wiki moja toka alipokamatwa na vyombo vya usalama nchini Tanzania.
Awali maafisa wa polisi na wale wa idara ya uhamiaji walisema anachunguzwa kuhusu utata wa uraia wake.
Baadae mawakili wake walitoa taarifa wakieleza mteja wao atashtakiwa kwa kuhusika na ripoti iliyochapiswha katika jarida la The Economist, lakini mahakamani kibao kikageuka tena na kuwa kesi ya ubadhirifu wa kiuchumi.
Makosa aliyoshtakiwa nayo hayana dhamana na ataendelea kusalia rumande mpaka mwisho wa kesi yake. Agosti 19, kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa tena mahakamani