Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 9:34 am

NEWS: MAREKANI IMESEMA IKOTAYARI KUPAMBANA KIVITA NA KOREA KASKAZINI

New York: Nchi ya Marekani , imesema kuwa itatumia nguvu za kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini “iwapo itahitajika kufanya hivyo, kauli hiyo imesemwa kupitia ubalozi wake katika Umoja wa Mataifa Bi Nikki Haley Kauli hiyo inakuja siku mbili tu baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio la kombora la masafa marefu linalotoka bara moja kwenda hadi bara jingine.


Bi Haley alisema siku ya Jumatano kwamba jaribio la kombora la masafa marefu la Korea Kaskazini ICBM linaangamiza suluhu ya uwezekano wa mazungumzo ya kidiplomasia.

''Marekani imejiandaa kutumia uwezo wake wote kujilinda na washirika wetu'', Bi Haley aliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo lilikutana kwa kikao cha dharura kuzungumzia hatua hiyo ya Korea Kaskazini.

Bi Haley ambaye alisema alijadili swala hilo na rais, alisema kuwa Marekani pia inaweza kukata biashara na mataifa ambayo yanaendelea kufanya biashara na Korea Kaskazini kwa kukiuka maamuzi ya Umoja wa Mataifa.

Korea Kaskazini ilifanya jaribio hilo ambalo linakiuka marufuku ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, licha ya vitisho vya Marekani na Umoja wa Mataifa.

Hivi karibuni Marekani ilisema kuwa haitokubali Korea Kaskazini kuendelea kukiuka sheria kwa kufanya jaribio la makombora yanayokiuka marufu ya Umoja wa Mataifa.

Nikki Haley alisema kuwa maamuzi mapya pia yatawasilishwa dhidi ya Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa, huku akilezea jaribio hilo kama tishio la kijeshi dhidi ya Marekani na dunia kwa ujumla. Baloi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa ametishia kutumia vikwazo vya kibiashara.