Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 7:56 am

NEWS: MAPENDEKEZO YA UCHAGUZI WA URAIS BOLIVIA YAWASILISHWA BUNGENI

Rais wa mpito wa Bolivia Jeanine Anez jana amewasilisha bungeni muswada wa sheria utakaowezesha kufanyika uchaguzi mkuu mpya baada ya kujiuzulu kwa Evo Morales kutokana na maandamano ya umma.

Lage in Bolivien Jeanine Anez (picture-alliance/dpa/AP/N. Pisarenko)

Wabunge wameanza kujadili mapendekezo hayo ambayo pia yanalenga kuchagua tume mpya ya uchaguzi na kuutangaza uchaguzi uliofanyika Oktoba 20 kuwa batili kufuatia tuhuma za wizi wa kura.

Anez ameahidi uchaguzi mpya utafanyika mapema iwezekanavyo na kuongeza kuwa anataka tume mpya ya uchaguzi itokane na maridhiano kati ya makundi ya raia nchini Bolivia.Morales alijiuzulu siku 10 zilizopita na kwenda uhamishoni nchini Mexico baada ya kuzuka madai ya wizi wa kura kwenye uchaguzi ambao ulimtangaza mwanasiasa huyo wa mrengo wa shoto kuwa mshindi.