Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 4:10 am

News: Manyanya jumla ya shilingi milioni 13.4 zimetumika kulipa madeni ya fedha za likizo kwa watumishi 6 wa chuo cha Ualimu Korogwe

Dodoma: Jumla ya shilingi bilioni 10.5 zimelipwa kwa walimu 22,420 katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2016/2017 hadi kufikia mwezi machi mwaka 2017.

Idadi hiyo ilifanya jumla ya walimu waliolipwa katika kipindi hicho kufikia elfu 86,234.

jumla ya shilingi bilioni 22.629 zililipwa kwa walimu elfu 63,814 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016 hadi juni 2016.

Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia mhandihi STELA MANYANYA amesema hayo leo mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Korogwe Vijijini MARRY CHATANDA aliyetaka kujua mpango wa serikali wa kuwapandisha daraja wale wanaostahili na lini serikali italipa madai yao ya fedha za likizo ambazo hawajawahi kulipwa.

Akijibu maswali hayo mhandisi MANYANYA amesema katika malipo hayo jumla ya shilingi milioni 13.4 zimelipwa kwa ajili ya madeni ya fedha za likizo kwa watumishi 6 wa chuo cha Ualimu Korogwe.

Amesema wizara inaendelea na uhakiki wa madeni ya miaka ya nyuma na kuratibiwa na mamlaka husika na taratibu za malipo zitakamilishwa kwa wale watakaostahili.