Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 5:35 am

NEWS: MANUKATO YA AIR FRESH YAWAKURUPUA WABUNGE

SHUGHULI za Bunge zimelazimika kusimama kwa muda baada ya kutokea hali ya taharuki ndani ya ukumbi wa bunge, baada ya kulia king’ora kinachoashiria na hali ya hatari na kusababisha wabunge kutoka nje bila kufuata utaratibu huku wakipiga kelele.

hali hiyo imetokea majira ya saa 10.58 wakati wa kipindi cha maswali na majibu muda mfupi baada ya Naibu Spika Dk.Tulia Akson kuuliza swali la Nyongeza kwa Naibu Waziri Maji na Umwagiliaji Jumaa Awesso na alipoanza kujibu ghafla king’ola kinachoashiria hatari kuanza kulia na kusababisha wabunge kuanza kuiga kelele na kukimbia kutoka ukumbi wa bunge na kwenda nje.


Kutokana na hali hiyo wabunge walianza kupiga kelele kwa kusema kuwa hatari, hatari na bila kufuata utaratibu unaotakiwa na kusababisha Mwenyekiti wa Bunge, Najima Giga kutangaza kuhairisha shughuli za Bunge.


Kwa mujibu wa kamanda wa zimamoto mkoa wa Dodoma amesema chanzo cha king'ora hicho kulia ni kutokana namanukato ya Air fresh yaliyopuliziwa bungeni.


Hii ni mara ya pili kutokea kwa hali ya sintofahamu ndani ya ukumbi wa Bunge kwani wiki mbili zilizopita kulitokea mtafuruku baada ya kuingia bundi ndani ya bunge jambo ambalo halijawahi kutokea tangu kujengwa kwa ukumbi huo.