- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MANJI APOKONYWA MALI YAKE NYINGINE NA SEREKALI
Dar es salaam: Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli amefuta umiliki wa shamba la Mfanyabiashara maarufu nchini Yusuph Manji la hekari 715 lililopo katika wilaya kigamboni Jiji Dar es salaam, kwa madai ya kushindwa kuliendeleza shamba hilo. Pia Rais amefuta umiliki wa shamba lingine la kampuni ya Amadol lenye hekari 5,400 katika wilaya hiyohiyo ya kigamboni.
Shamba hilo Manji alitaka kulitoa kwa yanga na lilikuwa kwenye mipango ya wanajangwani kupewa kujenga kiwanja cha kisasa Mpira, ambapo klabu ya yanga ingekuwa na umiliki wa uwanja huo.
Hili limekuwa ni pigo lingine kwa mfanyabiashara Yusuph Manji kupoteza mali zake kipindi hichi cha awamu ya tano, ambapo serekali ilifuta umiliki wa shamba lake la morogoro, pia alinyanganywa umiliki kiwanda cha ngozi kilichopo mkoani mwanza, Pia alishindwa kesi ya tigo, ambapo Kwa mujibu wa wanasheria wa majini wanasema kuwa majini alikuwa anamiliki hisa asilimia 72 za umiliki wa tigo,