Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 1:23 am

NEWS: MANISPAA YA UBUNGO YAPITISHA BAJETI YA TSH. BILIONI 84

Dar es salaam: Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imepitisha Makadirio ya bajeti kwa mwaka 2019/2020 ambapo imepanga Kutumia Kiasi cha Tsh Billioni 84.6 katika mamba mbali mbali yanayohusu Manispaa hiyo.

Hayo yamesemwa leo na Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo,Mh Boniface Jacob, wakati wa kusoma bajeti hiyo, amesema atika pesa hizo serikali itatoa ruzuku ya Billioni 65.5,Millioni 750 ni michango ya Wananchi na billioni 18.4 ni Makusanyo ya ndani.

Ambapo katika matumizi yake fedha hizo,Billioni 72.3 ni Mishahara ya watumishi,Na kiasi cha billioni 12.3 zimeelekezwa katika miradi Mbalimbali ya Maendeleo Aidha ameweka msisitizo kuwa Kiasi cha billioni 8.3 sawa na Asilimia 60,za mapato yanayokusanywa na Halmashauri zitatumika kwa ajili ya Miradi ya maendeleo

Mstahiki meya ametaja Vipaumbele 11 vya Halmashauri vilivyomo katika Bajeti hiyo ambapo ni pamoja na kuboresha utoaji huduma kwa jamii kwa kuongeza pesa za kujengea Makao makuu ya Halmashauri kiasi cha Millioni 700, kipaumbe kingine ni Kuanza kujenga Hospitali ya wilaya kwa kiasi cha Tsh Millioni 250

pia Manispaa hiyo imezamiria Kutenga fedha za kujenga machinjio ya kisasa kiasi cha Tsh Millioni 250

Kutenga fedha Kwa ajili ya ujenzi wa Soko la Mbezi( kwa ajili ya wamachinga) Kiasi cha Tsh millioni 300 - Kuimarisha Utawala bora kwa kuwatengea fedha za kiinua Mgongo wenyeviti wa Serikali za mitaa wanaomaliza muda wao mwaka 2019

Kuongeza Mapato kwa kuboresha miundombinu ya ukusanyaji,kubuni vyanzo vipya,Uanzishaji wa stendi za daladala Mloganzila na Msumi,Uanzishwaji wa Masoko mapya Kiasi cha Tsh Billioni 1.7 zimetengwa - Kuongeza kiwango cha Uzoaji taka Ngumu kwa manispaa kwa Kununua Vifaa vya ubebaji taka kama magari na mitambo,Kiasi cha Tsh billioni 3.02