- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MANISPAA YA DOM KWA MARA YA KWANZA YAPATA MEYA MSOMI
DODOMA: HATIMAYE Manispaa ya DODOMA imefanya uchaguzi wa Meya wa Manispaa hiyo Prof David Mwanfupe ambaye ni diwani wa kuteuliwa.
Prof.Mwanfupe amekuwa diwani kutokana na kuteuliwa na chama chake cha CCM kuwa diwani wa manispaa ya Dodoma.
Jumla ya kura zilizopigwa ni 58 ambapo Prof.Mwanfupe amepata kura 50 na diwani wa chadema Yona Kusaja amepata kura 8.
Akitangaza matokeo hayo Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwini Kunambi amesema wapiga kura wote ni 58 na hakuna kura iliyoharibika na Prof.Mwanfupe ameibuka na ushindi wa kura 50 na diwani Chadema amepata kura 8.
Kunambi amemtangaza Prof.Mwanfupe kuwa Meya wa Dodoma ikiwa anachukua nafasi ya Meya wa awali Jafary Mwanyemba ambaye aliondolewa kwa nafasi hiyo kwa kupigiwa kura na madiwani wenzake kwa madai kuwa hawakuwa na imani naye.
Hisia ya kutokuwa na imani na Mwanyemba iliibuliwa na madiwani wa upinzani na kuungwa mkono na madiwani wa CCM na kupelekea kupiga kura ya kutokuwa na imani naye nakumuondoa katika nafasi yake.
Wakati huo huo Mkuu wa wilaya ya Dodoma Manispaa Christina Mdeme ameapa kuhakikisha anakilinda na kukisimamia chama cha mapinduzi licha ya kuwa siyo mwanasiasa.
Kauli ameitoa leo alipokuwa akitoa neno la shukrani muda mfupi baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa madiwani.
Akizungumza mbele za madiwani Mdeme amesema kuwa yeye atahakikisha anasimamia utekelezaji wa CCM bila kuwa na hofu yoyote.
Naye mgombea umeya kupitia chama cha Chadema Yana Kusaja amesema licha ya kuwa kura zake hazikutosha lakini kura alizopata ni muhimu zaidi.
Amesema ili Dodoma iweze kusonga mbele ni lazima kufanya kazi kwa kutofuata mashinikizo ndani ya chama anachotoka.
Amesema prof.Mwanfupe anatakiwa kutumia elimu yake ili kuifanya manipaa ya Dodoma kuwa na maendeleo badala ya kuwa na makundi au kujenga chuki kati ya diwani na diwani.
Naye Meya wa Manispaa ya Dodoma Prof.Mwanfupe akitoa salamu za shukrani kwa baraza la madiwani amesema yeye hawezi kufanya kazi vizuri kama hatapata ushirikiano na madiwani wenzake.
Mbali na hilo amewataka madiwani wote kuondokana na mitazamo ya kiitikadi na badala yake wajenge tamaduni ya kufanya kazi za maendeleo kwa faida ya wananchi wote.
Baada ya kumalizika kupiga kura madiwani wa chadema wamesema kuwa wamesalitiana katika kupiga kura.
Malumbano ya madiwani hayo yametokana na kupigwa kura 8 kati ya 9 za madiwani wote wa Chadema.
Akizungumza na MUAKILISHI ,diwani wa viti Maalum Chela Mahula amesema wanatoa siku tatu za kufanya upelelezi wa kumtambua aliye wasaliti wenzake na atakapopatikana chama kitamwajibisha.