- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MANCHESTER CITY YAITENGENEZEA LIVERPOOL UBINGWA EPL
England: Club ya Manchester City imefifiza ndoto zake za kutetea ubingwa wa Premier league(EPL) baada ya kukubali kichapo cha mabao 2 - 1 mbele ya Newcastle Jumanne ya Jana usiku na kuipa nafasi Liverpool ya kufanya vizuri zaidi leo.
City walikuwa ugenini katika uwanja St James' Park, na waliuanza mchezo kwa kasi na kupata goli la utangulizi katika sekunde ya 24 ya mchezo kupitia mshambuliaji raia wa Argentina Sergio Aguero.
Baada ya City ulinzi wake kulegea ulimpa nafasi Salomon Rondon katika dakika ya 66 kufunga goli maridhawa akiunganisha pasi ya kichwa kutoka kwa Isaac Hayden.
Mchezo huo ulibadili muelekeo katika dakia ya 78 baada ya Newcastle ama maarufu kwa jina la Magpies walipata penati baada ya kiungo wa City Fernandinho - kumfanyia madhambi Sean Longstaff kwenye eneo la hatari.
Matt Ritchie alisubiri kwa takriban dakika mbili kabla ya kupiga mkwaju wa penati wakati kipa wa City Ederson akipokea matibabu.
Mkwaju huo ulipigwa katika dakika ya 80 na ulipeleka kilio kwa mashabiki wa City.
Sasa Man City wanapeleka matumaini yao kwa klabu ya Leicester City ambao wanapambana na vinara Liverpool leo Jumatano usiku. Iwapo Liverpool watashinda mchezo wa leo, basi watatanua pengo la uongozi wa EPL kwa alama saba.