Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 1:43 pm

NEWS: MAMLAKA ZA HALI YA HEWA EAC ZATOA ONYO MVUA KUBWA KUNYESHA

Mamlaka za utabiri wa hali ya hewa katika nchi za Afrika Mashariki, hasa nchini Kenya, Rwanda na Tanzania, zimeonya kuwa mvua kubwa zitaendelea kunyesha hadi mapema mwaka ujao, 2020 wakati huu maafa na madhara yakiripotiwa katika nchi za Tanzania na Kenya.

Mvuo hizo zimekuwa zimekuwa zikinyesha kwa kipindi cha wiki moja sasa na kusababisha maafa.

Nchini Tanzania watu 29 wamepoteza maisha katika mikoa ya Tanga na Morogoro, huku Kenya ikishuhudia vifo vya watu wanane.

Mamlaka katika nchi hizo za Afrika Mashariki, zinasema kuwa mvua zitaendelea kushuhiwa gadi mapema mwezi Februari mwaka 2020.

Iwapo hali hiyo itaendelea kushuhudiwa, basi huenda vifo zaidi vikashuhudiwa lakini pia mlipuko wa magonjwa kama kipindupindu.

Mataifa ya Afrika Mashariki, huwa yanashuhudia kipindi kifupi cha mvua kati ya mwezi Oktoba na Novemba.

Hali mbaya ya miundo mbinu katika nchi hizo zimeendelea kusababisha mafuriko