- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAMLAKA YA MAJI TANGA KUANZA KUTUMIA MITA ZA GPS, ZINAZOJISOMA ZENYEWE
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Tanga (Tanga Uwasa), imesema inampango wa kuanza kutumia mita za kisasa zenye mfumo wa GPS ambazo zitakuwa na uwezo wa kujisoma zenyewe uniti za maji zilizotumika kwenye mita ya Mteja.
Taarifa hiyo ilitolewa juzi na Ofisa Ankara wa Tanga Uwasa, Daudi Mkumbo, wakati akizungumza kwenye mkutano na wananchi wa Kata ya Duga jijini Tanga kutoa elimu kuhusu huduma zao.
Mkumbo alisema mita hizo zitakuwa zimefungwa chombo ambacho kitakuwa na uwezo wa kujisoma zenyewe hali ambayo itarahisisha usomaji.
Alisema anaamini uwepo wa mita hizo utaondoa changamoto kwa baadhi ya wateja ambao wanadai wasomaji hawafiki maeneo yao.
“Kwa sasa kuna teknolojia ambayo mtu hataweza kusoma mita ya maji kwa umbali wa mita zaidi ya 600, ina maana ndani ya 600 ndio mtu anaweza kusoma. Maana yake kila mita ya maji itakuwa imefungwa kifaa hicho cha GPS ya eneo na ile mita ilipo atakuwa anatambulika na msomaji akifika ndani ya mita 600 hawezi kudanganya,” alisema.
Alishauri wananchi wa maeneo hayo kuacha tabia ya kutokuacha mabomba wazi wakati wanasubiri maji kwani hiyo ndiyo inaweza kuwa chanzo kikubwa cha kupata bili kubwa ambayo haihusiani na matumizi ya maji.
“Kipindi ambacho maji yamekatika bomba linajaa upepo, hivyo wakati maji yanaporudi yakiwa na msukumo ule upepo ndio ambao unatangulia kabla ya maji unaozungusha mita na hiyo ndio chanzo cha bili kuwa kubwa. Ukifungulia maji wakati hamna maji utasababisha bili kuwa kubwa wakati maji yanaporudi huo ni ushauri,” alisema.
Mmoja wa wananchi wa eneo hilo, Selemani Rashid alishauri; “muweke utaratibu kwamba wasomaji wanapokwenda kusoma mita, wakutane na wahusika ili washuhudie namna zinavyosomwa ili kuonda dhana kwamba hawapiti.”