- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAMBOSASA MARUFUKU MADEREVA WA MAGARI YA SERIKALI KUPAKI BAR
DODOMA: JESHI la Polisi Mkoani Dodoma linawashikilia watuhumiwa 12 kwa makosa mbalimbali kufuatia msako mkali wa uhalifu unaondelea katika Mkoa Dodoma.
Hayo yameelezwa leo Mjini Dodoma na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma,LAZARO MAMBOSASA wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Kamanda MAMBOSASA amesema kuwa katika msako huo wameweza kukamata mali mbalimbali za wizi ikiwemo Pembe za Ndovu katika maeneo tofauti ya Wilaya za Mkoa wa Dodoma.
Aidha amewataka wakazi wa Mkoa huo ambao waliibiwa mali zao kujitokeza ili kwenda kuzichukua.
Hata hivyo Kamanda huyo ametoa rai kwa wakuu wa Taaisis na Idara za Serikali zikiwemo Wizarakuwaelekeza madereva wa magari ya Serikali na Pikipiki kuwa ni marufuku kwa magari ya Serikali kuegesha kwenye bar nyakati za usiku na madereva hao kuendelea kulewa pombe hadi usiku kwani wakibainika watachukuliwa hatua za kisheria.