- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAMBO 10 ALIYOYAONGEA RAIS MAGUFULI KWA WATENDAJI WA KATA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Septemba 2, 2019 amekutana na kufanya nao mazungumzo maafisa watendaji wa kata wote nchini.
Rais Magufuli ameongea nao mambo 10 muhimu katika Ustawi wa Maendeleo ya Tanzania
1.Nawahakikishia kuwa cheo cha Afisa Mtendaji Kata siyo kidogo, ninyi ni wawakilishi wangu na nawahakikishieni tembeeni vifua mbele na kamwe asitokee mtu wa kuwanyanyasa huko mliko.
2. Nimewaita tusalimiane, tujadiliane namna bora ya kutimiza wajibu wenu katika maeneo yenu mnakotoka, sina hakika katika maisha yenu kama mmeshawahi kuitwa na Wakuu wa Wilaya ama Wakurugenzi wa Halmashauri,kujadili kwa pamoja utendaji kazi wenu.
3. Najua mmekua mkionewa, mmekua mkihamishwa hovyo hovyo kwa utashi wa wakubwa wenu na nasema ni marufuku kwa Afisa Mtendaji Kata kuhamishwa bila kufuata taratibu.
4. Hiki ni kikao muhimu sana ndiyo maana nataka tuzungumze na kujadiliana juu ya utekelezaji wa majukumu yenu ya kila siku kwakua ninyi ndiyo mko karibu na wananchi na hakuna anayezielewa na kuzijua changamoto za Vijiji na Kata nchini zaidi yenu.
5. Mna majukumu ikiwemo kuhakikisha usalama katika maeneo yenu, Amani ndiyo msingi wa maendeleo lakini nasistiza hususani kwa kata zilizoko mpakani, watambueni wageni wanaoingia mipakani na hakikisheni hawapati vitambulisho vya uraia ambavyo zoezi la kuvitoa kwa wananchi linaendelea.
6.Kutatua kero za wananchi ni jukumu lenu lingine, jiwekeeni utaratibu wa kukutana na wananchi na siyo kusubiri wananchi wabebe mabango wakati wa ziara ya Rais na kama hamtasikiliza na kutatua kero za wananchi uwepo wenu katika maeneo yenu hautakua na maana.
7. Kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika kata zenu ni jukumu lenu na kamwe msikubali mradi kutekelezwa chini ya kiwango kwani na wewe utahusika, wewe ni bosi hupaswi kukaa pembeni wakati pesa zinachezewa.
8. Natoa rai kwa baadhi yenu, taarifa ninazo acheni kua madalali wa kuuza ardhi kwani ndio chanzo cha migogoro ya ardhi nchini, wacheni kujihusisha na vitendo vya rushwa na dhuluma, mnabambikia wananchi kesi, hamna huruma hata kwa wajane na yatima.
9.Siku zote mtangulizeni Mungu,mnaposhughulika na maisha ya wananchi, mkumbuke maisha mliyoanza nayo.