Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 5:41 am

NEWS: MAMA TUNU PINDA: ''VIONGOZI WA SERIKALI IGENI MFANO WA MZEE PINDA ''

DODOMA: Wito umetolewa kwa viongozi wa serikali kujishugulisha katika kilimo ili kuweza kuupa mwili mazoezi pamoja na kuonyesha mfano kwa wananchi kuwa kilimo ni shuguli inayothaminiwa.

Hayo yameelezwa na Mke wa Waziri mkuu mstaafu wa awamu ya nne Mama Tunu pinda wakati alipokuwa akitoa taarifa kuhusu shamba la waziri mkuu msaafu Mizengo Pinda wakati wa Mbio za mwenge wa uhuru ulipofika kata ya Zuzu nje wilaya ya Dodoma mjini anapoishi waziri mkuu mstaafu

Mama Tunu amesema kuwa kuanzisha shamba kwa watumishi na viongozi wa serikali kuna changamoto nyingi ikiwemo kuamishwa kikazi lakini hilo si tatizo kwa sababu unaweza kutumia eneo hilo hata baada ya kustaafu katika ajira yako.

Amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa shamba hilo kumekuwa ni kivutio kikubwa kwa viongozi mbalimbali wa kisiasa wananchi pamoja na makundi mbalimbali kwenda katika shamba hilo kwa ajili ya kujifunza pamoja na taasisi za elimu na mawaziri .

Kwa upande wake Naibu waziri na Mbunge wa Dodoma Mhe. Antony Mavunde amemshukuru Mzee Pinda kwa jitihada zake anazoendelea kuzifanya kwa kutoa hamasa hata kwa viongozi wengine kuweza kujifunza kutoka kwake.