Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 1:27 am

NEWS: MAMA MZAZI WA ERICK KABENDERA AFARIKI DUNIA

Mama mzazi wa mwandishi wa habari Erick Kabendera, Bi Verdiana Mjwahuzi amefariki Dunia leo Desemba 31, 2019 katika Hospitali ya Amana Jijini Dar es salaam na Mazishi yanatarajiwa kufanyika nyumbani kwake Chang’ombe na mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali hiyo ya Amana.

Bi Mjwahuzi amefariki Dunia akiwa na Umri wa miaka 81.

Kama utakumbuka Desemba 13, mwaka huu mama huyo alizungumza na waandishi wa habari akimuomba Rais Magufuli amsamehe mwanaye kwani ndiye aliyekuwa akimtegemea kwa kila jambo ikiwepo gharama za matibabu yake na Uwangalizi wake.

Erick Kabendera alikamatwa mwezi Julai 2019 na kukabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha, kukwepa kodi na kuongoza kikundi cha uhalifu. Mashtaka ambayo mawakili wake wameyakana.

Kabendera ni mwandishi wa habari za kichunguzi ambaye amefanya kazi na vyombo vingi vya habari vya ndani na nje ya nchi

Watu wengi wameguswa na kesi ya Kabendera wakiwemo wanaharakati wa haki za binadamu ambao wameielezea kama muendelezo wa uminywaji wa uhuru wa habari na haki ya watu kujieleza nchini

Wiki iliyopita wakili wa Kabendera aliuhoji upande wa mashitaka juu ya kuchelewa kujibiwa kwa barua ya Kabendera iliyokwenda ofisi ya DPP kuomba kuanza kwa majadiliano ya kukiri makosa na kuomba msamaha