Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 7:32 am

NEWS: MAMA AMCHINJA MWANAE WA MIEZI SITA.



MANYARA: Jeshi la Polisi mkoani Manyara , linamshikilia mwanamke mmoja kwa tuhuma za kumuua kwa kumchinja kwa kisu mtoto wake wa kumzaa wa miezi sita Flora Theophil.

Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara Agustino Senga amesema tukio hilo limetokea Januari 20.2019 katika Kijiji cha Kisimani katika wilaya ya Simanjiro ambapo mama huyo Sesilia Paskali [29] aligombana na mume wake kwa kile kinachoelezwa kuwa ni wivu wa kimapenzi kwamba amekuwa akipokea simu ya mumewe,ikisikika sauti ya mwanamke ambaye hamfahamu na kuhisi ana mahusiano nae hali iliyopelekea ugomvi huo na kusababisha mwanaume kuondoka nyumbani na kurudi baada ya kusikia taarifa ya mauaji hayo siku ya jumapili.

Kamanda Senga aliendelea kueleza kuwa baada ya mwanamke huyo kutenda tukio hilo alitaka kujiua kwa kunywa vidonge vingi lakini jaribio hilo likafeli baada ya majirani kumuokoa na kumkimbiza hospitali ambapo kwa sasa anaendelea kupata matibabu akiwa chini ya ulinzi wa polisi.

Katika tukio lingine kamanda amesema Januari 18 mwaka huu mwanaume mmoja aliefahamika kwa majina Mandela Nada [28] alikutwa akiwa amepoteza maisha baada ya kusombwa na maji yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika kata ya Bargish tarafa ya Daudi wilaya ya Mbulu na mwili wake umeshachukuliwa na ndugu zake kwa ajili ya mazishi.