- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MALINZI AJITETEA HAJAWAHI KUJAZA FUMO YA KULALAMIKA KULIPWA FEDHA
ALIYEKUWA Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi ameieleza mahakama ya hakimu mkazi kisutu kuwa alikuwa akilipwa fedha na TFF kwa taratibu za uendeshaji wa shirikisho hilo na wala hajawahi kujaza fomu ya madai ya ulipwaji wa fedha na wala hajawahi kutoa maelekezo ya jinsi ya upokeaji wa fedha hizo.
Malinzi ameeleza hayo leo Septemba 18,2019 mbele ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde wakati akijibu maswali ya wakili wa serikali kutoka Takukuru Leonard Swai.
Amedai kuwa fedha hizo zililipwa kupitia kwa Shadi wa 10 Hellen Ushahidi wa 12 Miriamu Zayumba na nyingine zilikuwa zikiingizwa kwenye akaunti.
Amedai katika shtaka la 16-25 inaonyesha kuwa alilipwa fedha na TFF, lakini fedha hizo zililipwa kwa utaratibu na sio kweli kwamba aliwahi kutoa maelekezo ya upokeaji wa fedha hizo na kuongeza kudai kuwa, hundi na vocha zilizotolewa mahakamani ni baadhi kwani kuna zingine hazikuletwa mahakamani kama ushahidi.
Akiendelea kutoa ushahidi alidai aliwahi kufadhili mbio za wabunge (bunge marathon) kwa mika 7 toka miaka1997 hadi 2004 kuutangaza mchezo wa ngumi,mchezo wa golfu pamoja na kujenga uwanja.
Amedai wakati anafadhili mbio hizo, Spika wa wakati huo pamoja na mwenyekiti wa bunge hawakumbuki ila anayemkumbuka ni kiongozi wa timu hiyo marehemu Joeli
Bendera na baadae alifuatiwa na William Ngeleja na kwamba fedha zilitoka Cargo Star na nyaraka za kumkabidhi fedha Bendera na Ngeleja zipo Cargo Star.
"Fedha hizo kwenye risiti zilikuwa zikiandikwa kulipwa mkopo na nyingine marejesho ya mkopo na wala sikuwahi kumkabidhi mtu yoyote nyaraka za malipo" amedai
Malinzi bado anaendelea kuhojiwa kutokana na ushahidi wake wa utetezi, kesi hiyo itaendelea kesho
Mbali na Malinzi, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa, Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga na Karani Flora Rauya.
Katika kesi hiyo ya jinai namba 213 ya mwaka 2017 washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 20 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa Dola za Marekani 173,335.