Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 6:03 am

NEWS: MALAWI KUWAGAWIA WANANCHI WAKE ELFU 90 KILA MWEZI

Rais Arthur Peter Mutharika wa Malawi amsema taifa lake litazindua mradi wa dharura wa kusafirisha fedha ambao unatarajiwa kuwalenga watu milioni moja pamoja na wafanyabiashara wadogo waliathiriwa na janga la virusi vya corona. Kwa kupitia mpango huo kaya zinazostahili zitapokea kiasi cha kwacha elfu 35 fedha ya Malawi, ikiwa sawa na dola 40 kwa mwezi, ikilinganishwa na kiwango cha chini kabisa cha mshahara nchini humo.

Peter Mutharika sworn in as Malawi's president

Katika hotuba yake ilioneshwa kupitia televisheni ya umma, Rais Mutharika pasipo kueleza mpango huo unaotarajiwa kuanza Mei, utadumu kwa muda gani, amesema hatua hiyo itatoa unafuu wa maisha ya watu wengi wa taifa hilo. Malawi ambayo imekuwa katika mkwamo wa kiuchumi katika miaka ya hivi karibuni ina visa 36 vya maambukizi ya corona na vifo vitatu.

Juma lililopita Benki ya Dunia imeridhia kitita cha dola milioni 37 milioni kwa lengo la kuisaidia Malawi kukabiliana na janga la corona. Hata hivyo upinzani na makundi ya kupiginia haki za binaadam yamemkosoa Mutharika kwa kufanya upendeleo wa kivyama