- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAKONDA "MARUFUKU KUINGIA MJINI UKIWA MCHAFU"
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amepiga marufuku 'watu wachafu' kuonekana mitaa ya mjini ya jiji hilo katika kipindi cha mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Kauli hiyo ya Makonda ameitoa leo Julai 29, 2019 wakati akizungumza na Waandishi wa habari juu ya Mkutano wa 39 wa SADC unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao, Agosti 18 na 19 nchini Tanzania katika jiji la biashara la Dar es salaam.
Kama sehemu ya maandalizi ya mkutano huo, Bwana Makonda amesema jiji hilo leye wakaazi wengi zaidi nchini Tanzania litakuwa katika hali ya usafi mkubwa.
"Tabia ya kuja mjini bila kunyoosha nguo ni marufuku. Tabia ya kuja mjini hujaoga ni aibu. Watu wanatembea tu na chawa, kama huwezi kuwa msafi basi subiri mwezi huu upite," Makonda
"Kwa kipindi hiki tuvumiliane, kama hufui nguo, kama huogi, pumzika kidogo kuja mjini." amesema Makonda
Sababu ya kutoa amri hiyo kwa mujibu wa mkuu huyo wa Mkoa ni kuepuka "kumtia aibu Rais wa Tanzania John Magufuli mbele ya marais kutoka nchi 15 watakaokuwa hapa nchini."
Pia, Makonda ameagiza kwamba mtu yoyote mwenye gari atakayetupa takataka barabarani asitozwe faini badala yake apewe eneo la kufanya usafi. Amesema baadhi ya watu hao wana jeuri ya fedha, hivyo kwao faini siyo adhabu.
"Mtu mwenye gari akitupa takataka msimtoze faini, mshusheni kwenye gari, mpeni kipande cha kilomita moja cha barabara apige deki. Hawa watu fedha kwao siyo tatizo, sasa tunataka kuwaonyesha kwamba na sisi tuko 'serious' na usafi wa jiji letu.
hughuli za usafi katika jiji hilo kwaajili ya mkutano wa SADC zinatarajiwa kuanzia leo kuendeshwa na vijana 130 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na mgambo 300 katika maeneo mbalimbali ya jiji.