- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAKONDA AWAKABIDHI YANGA NYARAKA ZA UWANJA WAO
Dar es Salaam. Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewakabidhi nyaraka za uthibitisho Club ya Yanga kuonyesha wao ni wamiliki halali wa uwanja huo uliopo Kigamboni Jijini Dar es salaam baada ya Juzi toa Ahadi ya kupatia Yanga Uwanja wao Binafsi.
Hafla ya kuwakabidhi cheti hicho cha utambuzi, imefanyika leo kwenye Hoteli ya Serena jijini ambako Makonda alikabidhi kwa mwenyekiti wa Yanga, Dk Mshindo Msolla.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi cheti hicho, Makonda alisema makabidhiano hayo yanatoa ishara njema kuwa serikali ina nia ya dhati ya kukuza michezo.
"Jumamosi iliyopita niliahidi kuipatia Yanga, uwanja eneo la Kigamboni na leo tumeanza mchakato wa kuwamilikisha Yanga eneo na siku ya Ijumaa rasmi eneo ili waanze ujenzi," alisema Makonda.
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Omary Kaya amemshukuru mkuu wa mkoa na serikali kiujumla kwa kuwapatia uwanja huo.
Kwa upande wetu sisi Yanga tunamshukuru Mkuu wa Mkoa kwani jambo alilolifanya ni kubwa kwa faida ya klabu yetu na taifa kwa ujumla.
“Tunangoja makabidhiano rasmi na baada ya hapo ndipo tutajipanga kuanza ujenzi wa uwanja," alisema Kaya