- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAKOMBORA 5 YAMEFYATULIWA KWENDA ISRAEL KUTOKA GAZA
Jeshi la Israel limesema makombora matano yamerushwa kutoka ukanda wa Gaza kuelekea Israel baada ya siku ya maandamano ya umma ambapo vikosi vya Israeli vilíwauwa Wapalestina wanne karibu na mpaka wa Palestina.
Shambulio hilo la makombora linatishia kudhoofisha hatua za upatanishi nchini Misri za kutafuta mkataba utakaopungaza vizuzizi vilivyowekwa na Israeli na Misri kwenye ukanda wa Gaza.
Hapakuwa na majeruhi kwenye shambulio hilo la leo na hakuna kundi lolote la Palestina liliodai kuhusika. Mamia kwa maelfu ya Wapalestina waliandamana kwenye ukanda wa Gaza siku ya Jumamosi kuadhimisha mwaka mmoja wa maandamano ya umma kwenye mpaka na Israel.
Makundi madogo ya wanaharakati yaliusogelea uzio wa mpaka na Israeli wakitupa mawe na vilipuzi kabla ya jeshi la Israeli kijibu kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi na kufyetua risasi zilizoua watu wanne na kujeruhi Wapalestina 64.