Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 11:04 pm

NEWS: MAKAZI BORA KUWA AGENDA YA KITAIFA.

DODOMA: Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jmaii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu amesema Serikali imeichukua Kampeni ya kuhamisha wananchi kujenga nyumba bora iitwayo “Piga Kazi: Boresha Makazi” kuwa Agenda ya kitaifa kwa miaka mitatu ijayo.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo jijini Ddooma mara baada ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu na Bajeti kwa kipindi cha nusu Mwaka (Julai-Disemba 2019) kwa kamati ya Bunge ya Kudumu ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa upande wa Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii.

Waziri Ummy amesema kuwa ni jambo ambalo Wizara limelihamasisha katika kipindi cha nusu mwaka ni kuchagua baadhi ya mikoa kuanza kwa mfanokujenga nyumba bora kwa wasioiweza na kuhamasiaha wanaojiweza kujenga ili iweze kusambaa nchini nzima ili kuwezesha wananchi kuboresha makazi yao.

Ameongeza kuwa Kampeni hii yenye Kauli mbiu “Piga Kazi: Boresha Makazi” inalenga kupunguza Kaya zenye makazi duni kwa silimia 50 kutoka asilimia 15.9 ya sasa hadi kufikia asilimia 8 ifikapo mwaka 2022

Aidha Waziri Ummy amesema wananchi wakiboresha makazi itasaidia kuondokana na maradhi mablimbali ikiwemo kifua kikuuu na kuwezesha jamii kuwa na sehemu salama za kulala hivyo kupunguza magonjwa yanayotokana na uchafu na kukosa hewasafi.

Kwa upande wake Mbunge wa Temeke Mhe. Abdallah Mtole amesema kuwa Tanzania ya Viwanda na Uchumi wa kati itawezekana ikiwa wananchi watahamasishwa kujenga nyumba bora kwani uchumi wa viwanda na wa kati unaanza na wananchi kuwa katika mazingira bora ya malazi.

Kupitia Kampeni ya kuboresha makazi imewezesha kufikia wakazi wa Kata ya Mzenga Kisarawe mkoa wa Pwani , Mpanda ndogo na Kabungu mkoani Katavi, Ikungi na Chibumagwa mkoani Singida na imelenga kufikia mikoa 26 ya Tanzania Bara.