Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 8:33 am

NEWS: MAKAMU WA PILI WA ZANZIBAR AWAASA WAANDISHI WA HABARI KUTUMIA VIZURI NAFASI YAO.

Zanzibar: Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema wandishi wa habari watumie vizuri kalamu zao na wanapo andika habari zao wazifanyie uchunguzi kwa makini isiwe kukurupuka kuzitangaza kwani zinaweza kuwaletea matatizo wao wenyewe ua kusababisha matatizo makubwa kwa taifa na jamii kwa ujumla.

Hayo ameyasema leo huko kilimani katika ukumbi wa chuo cha babari na masiliano katika maazimishi ya siku uhuru wa habari dunini.

Amsema Kumewahi kutokea matatizo mengi duniani yalio sababishwa na wandisha wa habari kwa kuitumia vibayo kalamu yao au kushabikia mambo bila utafiti jambo ambalo limesababisha maafa makubwa na kupelekea kupoteza roho za watu wasio nahatia katika mataifa yao.

Akitoa mfano wa baadhi ya taifa lilo kubwa na mkasa huo, alisema vita vya iraki nimoja ya mfano mmbaya ambao ulishabikiwa na wandishi wa habari kulazimisha iraki kumiliki silaha za sumu na kupelekea kuvamiwa kituambacho kilikuwa si kweli.

Amsema wandshi wajiepushe na masuala kama hayo kwani hilo nitatizo ambalo halite saulika katika historia ya binaadamu.

“Musishabikie tu kwa kuandika habari ambazo hamja zifanyia uchunguzi au mkatumiwa na watu kwamaslahi binafsi mtasababisha matatizo katika nchi au jammi husika ”alisema Balozi.

Aidha alisema kuwa serikali ya mapinduzi ya zanzbar ipo karibu sana na wandishi wa habari ndio maana hivi karibu Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dk.Ali Muhamed Shein aliwaita wandishi wa habari kwa nyakati tafauti na kuwataka watafute habari kwa viongazi wa serikali kila pale wanapo gundua kuna habari waende kudadisi.

Amsema mwandishi mzuri niyule anae tumia vyema kalamu yake naasie kubali kutumiwa na wana siasa,wafanya biasha na watu wengine kwa maslahiyao binafsi.