Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 12:59 am

NEWS: MAKAMU RAIS ZANZIBAR AWATAKA WATANZANIA KUZALIANA KWA WINGI

Makamu wa Pili wa Rais visiwani Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, amewataka wakazi wa Kahama na viunga vyake mkoani Shinyanga Nchini Tanzania kuzaliana kwa wingi kwa kuwa wana rasilimali za kutosha na Mkoa wao Kijografia ni mkubwa.

Image result for Balozi Seif Ali Iddi na waandishi

Balozi Seif aliyasema hayo alipotembelea Hospitali ya Mji wa Kahama na kuzungumza na wazazi waliojifungua pamoja na wauguzi, huku akisisitiza wauguzi wa hospitali hiyo kuwa la lugha nzuri kwa wagonjwa.

Alisema kitendo cha hospitali ya mji kuwa na idadi ya kuzalisha watoto 40 mpaka 50 kwa siku sio suala la kubeza, na kuongeza kuwa watoto hao baadaye wataongeza nguvu kazi katika kuzalisha chakula ambacho kitakuwa msaada katika familia wanazotoka na mkoa mzima. Akikabidhi msaada wazazi waliojifungua siku hiyo, mke wa Balozi Seif, Asha Suleiman, aliwataka wazazi kuvitumia vyema vifaa hivyo.

Alisema vifaa alivyotoa ni magodoro, vitanda, mashuka, taulo za kinamama 60, baiskeli za wagonjwa nne, kanga za kwa waliojifungua, maski gloves vikiwa na thamani ya shilingi milioni 3.1.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainabu Tellack, alisema Hopsitali ya Mji wa Kahama ina mahitaji makubwa ya vifaa tiba kwani wagonjwa wengi wanatoka katika halmashauri mbalimbali zilizopo jirani na wilaya kama Geita, Bukombe, Kaliua, Urambo, Nzega na Bongwe kuja kutibiwa.