- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAJIBU YA CAG MUSSA ASAAD KWA SPIKA NDUGAI
Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za serekali hapa nchini (CAG) Prof. Mussa Asaad amemtaka spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuheshimu katiba ya nchi.
Prof. Asaad amesema hayo baada ya kauli ya Spika Job Ndugai kumtaka kufika kwenye Kamati ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge,ili kuhojiwa na akamuonya kuwa asipofika kwa hiyari yake basi atapelekwa kwa Pingu.
Akijibu madai hayo na iwapo ataitikia wito wa Spika Ndugai ama atagomea, Prof. Asaad anasema, “umeuliza kama nitaitikia wito, sitajibu hilo. Ila naomba niweke rekodi sawa; ule siyo wito. Ni amri.”
Anasema, “…sasa kwa kuheshimu katiba yetu na kwa kuwa sitaki kuwa miongoni mwa waivunjao katiba, niseme hivi, Ibara ya 18 (a) inampa kila mtu uhuru wa kutoa maoni.
“Hivyo basi, kwangu mimi nachukulia hayo yote, kama mtu kaamua kutoa maoni yake na kuelezea fikra zake.”
Aidha, Prof. Asaad anasema, “jambo la pili, Ibara ya 26 (1), ya Katiba ya Jamhuri, inaelezea wajibu wa kila mtu kufuata na kutii katiba ya nchi.
“Sasa mimi nilidhani, mtu kama spika wa Bunge, alipaswa kuwa mfano bora katika kuhakikisha kuwa Ibara ya 143 ya Katiba, inayonitambua mimi na taasisi ninayoingoza, inaheshimiwa kama inavyostahiki.”
Prof. Asaad anasema, hatayumbishwa na kauli hizo wala vitisho alivyopewa. Bali anasema, “niseme tu, nitasimamia ninachokiamini kitaaluma na kwa uzalendo kwa maslahi mapana ya taifa letu.”
Kauli ya Prof. Asaad imekuja siku mbili baada ya Spika Ndugai, kuzungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma na kumtuhumu kiongozi huyo, kudhalilisha Bunge.
Spika Ndugai alikuwa akirejea kauli ya CAG, aliyoitoa nchini Marekani wiki iliyopita, kwamba mhimili huo wa kutunga sheria, umekuwa dhaifu mno na hivyo umeshindwa kutimiza wajibu wake.
Ndugai alitumia mkutano huo, pamoja na mengine, kuagiza Kamati ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge, kumhoji Prof. Asaad na baadaye kumshauri yeye hatua za kuchukua.
Akizungumza kwa hasira, Jumatatu iliyopita, mjini Dodoma, Ndugai alisema, Prof. Assad, anatakiwa kufika mbele ya kamati hiyo, tarehe 21 Januari 2019, ili kujibu “tuhuma za kudhalilisha Bunge.”
Amedai kuwa ameamua kuchukua hatua hiyo, baada ya kujiridhisha kuwa CAG ameliita “Bunge dhaifu.”
Amesema, “…ninamtaka CAG, kufika mbele ya Kamati ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge, kwa hiari yake, tarehe 21 Januari mwaka huu. Vinginevyo, nitaagiza akamatwe na kuletwa mbele ya kamati kwa pingu.” alisema spika.
#Chanzo mwanahalisi