- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAJASUSI WA MAREKANI CIA WAUWAWA NA CHINA
MAREKANI: Gazeti la New York Times limeripoti kuwa China, imewauwa au kuwafunga jela majasusi kati ya 18 au 20 hivi wa CIA, katika kipindi cha miaka miwili iliyopita na kulemaza kabisa shughuli za Marekani za kuichunguza China.
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Polisi wa China wakilinda ubaloziu wa Marekani katika mji mkuu, Beijing
Afisa mmoja mkuu wa Marekani ameliambia gazeti hilo kuwa, hiyo ni mojawapo ya ukiukaji mkubwa wa usalama, kwa miongo kadhaa na kufananishwa na usaliti wa kutoa siri kwa Urusi na Aldrich Ames (wa CIA) na Robert Hanssen (wa FBI).
Baadhi ya watu sasa wanadhani kuwa China, ilidukua mfumo wa mawasiliano wa CIA, ambayo hutumiwa katika mazungumzo ya kisiri.
Lakini kunao wengine wanaoamini kuwa, mdukuzi alisambaratisha kizuizi cha siri cha wapelelezi wa Marekani, mnamo mwaka 2010.
Majasusi hao walianza kutoweka mmoja baada ya mwingine, kuanzia mwanzo wa 2011 (huku mmoja wao akipigwa risasi mbele ya wenzake katika eneo la kubarizi, kwenye jumba la serikali).
Idara ya ujasusi CIA, imekataa kuzungumzia swala hilo.