Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 9:45 pm

NEWS: MAJAMBAZI WAIBA MASHINE YA ATM KWA KUTUMIA TINGATINGA

Image result for northern Ireland thief take ATM machine

Nchini Ireland ya Kaskazini kumetokea tukio lisilo la kawaida pale ambapo Majambazi wametumia tingatinga kunyofoa mashine ya kieletroniki kutolea pesa ( ATM) hiyo kutoka kwenye ukuta wa duka moja katika Kaunti ya Antrim.

Walter Millar at the shop

Tukio hilo limetokea baada ya wezi hao kuiba tingatinga hilo kwenye eneo la Ujenzi majira ya saa tisa ya usiku wa jana Jumatatu pia Polisi wamethibitisha kuwa jengo hilo limeharibiwa vibaya.

Mmiliki wa duka hilo bw. Walter Millar anasema awali alipopokea taarifa juu ya wizi huo, mmiliki wa duka hilo bwana Millar alidhani ni uzushi tu wa Siku ya Wajinga, Aprili mosi.

"Nachoweza kusema ni kuwa, wametumia tingatinga ambalo waliliiba kwenye eneo moja la ujenzi mwishoni mwa mtaa, wakainyofoa mashine na kuipakia kwenye gari na kuondoka nayo," amesema.

Image result for northern Ireland thief take ATM machine

"Ukuta wa jikoni umeharibiwa kabisa...tumekuwa na wakati mgumu, na ukijumlisha na hali ya kiuchumi iliyopo, vitu kama hivi vinatumaliza kabisa."

"Tulipokea simu kuhusu tukio hilo mishale ya saa 9:25 usiku kuwa tingatinga linaungua moto nje ya duka ambalo ATM imechomolewa," Inspekta wa Polisi Richard Thornton amesema.

"ATM imenyofolewa ukutani na kuharibu jengo ilipokuwa imewekwa...tunawataka mashuhuda wajitokeze, hususan walioiona gari ya rangi ya fedha."

Mwezi uliopita, polisi walitangaza kuundwa kwa kikosi kipya cha kupambana na wizi wa mashine za ATM.

Toka ulipoanza mwaka 2019, mashine saba za ATM zimeibiwa. Polisi pia wanaamini kuna makundi kadhaa ya majambazi ambayo yanajihusisha na wizi wa mashine hizo.