- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAJALIWA AONYA BARUA ZA SEREKALI KUVUJA MITANDAONI
Dodoma. Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameonya vikali tabia ya baadhi ya wafanyakazi wa Serekali kuposti barua za ofisi za Serekali mitandaoni, hasa katika mitandao ya Instagram na WhatsApp huku akitaka taarifa hizo kuwa siri.
Majaliwa ametoa kauli hiyo hii leo Jumatano Juni 30, 2021 katika mkutano wa mafunzo ya uongozi kwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala Tanzania Bara.
“Hiyo tabia imeibuka sana kwa miaka ya hivi karibuni tunapotumia mitandao yetu. Kwa hiyo kuna haja ya kudhibiti utandawazi uliopo na matumizi ya mitandao ya kijamii naamini kila mmoja wenu atakuwa makini sana kwenye mada hii,” amesema
Amesema kuwa siri ndio uhai wa Serikali akiwataka watendaji hao pale ambapo itawasilishwa mada kuhusu usiri kwa taarifa za Serikali wawe makini kusikiliza