- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAJALIWA : ACHENI KUFUATA MAINI
DODOMA: WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameonesha kukerwa na vitendo vya wataalam wa mifugo nchini (maafisa mifugo) kupishanana na pikipiki kwenda kupima nyama ili wapatiwe maini badala ya kutoa elimu kwa wafugaji juu ya ufugaji bora.
Majaliwa ametoa kauli hiyo juni 15 mwaka huu wakati akifungua mkutano uliowahirikisha maafisa mifugo,wataalam wa wizara ya Kilimo,walaalamu wa wizara ya viwanda pamoja na wataalamu wa wizara ya utalii na maliasili unaoendelea mjini Dodoma.
Waziri Mkuu amesema kuwa hayo ameyashuhudia wakati akiwa kwenye ziara katika baadhi ya mikoa ambapo katika ziara hiyo alionyesha wazi kutofurahishwa na namna ambavyo sekta ya mifugo inavyoongozwa kutokana na kukosekana mtaalamu wowote unaojitokeza kwa wafugaji wa mifugo.
Aidha amewataka wataalam hao kuhakikisha wanaleta mabadiliko katika sekta hiyoili kuwaongezea wananchi kipato na Taifa kwa ujumla badala ya kutumia utaalam wao katika kupima nyama kwa ajili ya matumizi.
Kuhusu kutenga maeneo ya wafugaji nchi waziri mkuu akatoa agizo kwa Halmashauri nchini kupitia mpango bora wa matumizi ya ardhi huku akisemakatika maeno hayo serikali inajipanga kufikisha miundombinu ikiwemo kujenga majosho.
Ikumbukwe kuwa Serikali inafanya jitihada ya kuangalia namna nzuri ya ujenzi wa viwanda kwenye maeneo mbalimbali ya nchini huku ikitoa wito kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi katika suala la uwekezaji wa kujenga viwanda hapa nchini.