- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAHOJIANO YA POLISI NA LOWASSA YAHAIRISHWA MPAKA JULY 13 2017
Dar es salaam: Waziri mkuu wa zamani na mjumbe wa kamati kuu wa chadema Taifa Eduward Lowassa leo aliitikia wito wa polisi ambapo, Polisi walimuita Mhe. Lowassa arudi tena leo Juni 29/2017, lakini leo ameambiwa arudi tarehe 13 Julai 2017 ambapo polisi wataendelea na mahojiaño na Lowassa tarehe hiyo baada ya ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa Serekali kutaka kuchunguza kama kuna chembe za uvunjifu wa amani kwenye hutuba aliyo itoa Lowassa juu ya kufungwa kwa Mashekhe nchini.
.
Naye Mbunge wa Hai Freeman Mbowe amelaani kitendo cha kutoruhusiwa kwa waandishi kwenye wito huo
"Na suala la kufukuza Waandishi wa Habari sio sawa, unapomuita Kiongozi wa kisiasa kama Mhe. Lowassa kwa Waandishi wa Habari ni hot story, wanayo haki ya kutaka kujua nini kinaendelea ili waweze kulipasha Habari Taifa kwani ni haki yao kupata taarifa." Aliongea Mh. Mbowe
"Waandishi wa Habari wanafukuzwa, wakati Polisi wakiwa na taarifa zao wanataka jamii ifahamu inawahita Waandishi wa Habari, lakini sisi viongozi wa Upinzani Waandishi wakija kuchukua Habari inaonekana kama ni kitu haramu."
Inabidi tuongee na Waandishi vichochoroni kama iliyotokea pale Makao Makuu ya polisi.
Polisi wasijaribu kutufunga midomo, ni kweli kuna Mashehee wako mahabusu kwa muda mrefu bila kupelekwa Mahakani. Hatutei uhalifu ukifanywa na Kiongozi yeyote awe wa kikristo au awe wa kiislam, kuna msemo wa Kiingereza unasema "Justice delayed is justice denied"
Na sisi kama Chama tunalaani mauaji yanayoendelea katika mkoa wa Pwani, hatuungi mkono na hatutetei mauaji yanayoendelea. Aliongea Mbowe