- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAHIGA "HATUJAWAHI KUINGILIANA KWENYE CHAGUZI ZETU NA KENYA"
Dar es salaam: Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , kikanda na kimataifa Dkt Augustine Mahiga amekanusha madai ya kwamba imekuwa ikiingilia uchaguzi wa kenya unaotarajiwa kufanyika agosti nane.
“Hatujawahi kuingiliana, Kenya haijawahi kuingilia Tanzania na Tanzania haijawahi kuingilia Kenya, leo kwa nini iwe hivyo?”
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam, Waziri Mahiga katika mkutano na waandishi, alikuwa na lengo la kuzungumzia pia vikwazo vya kibiashara baina ya Tanzania na Kenya vilivyoibuka hivi karibuni.
“Sisi tunautaratibu wetu wa Afrika Mashariki tunatembeleana, na tunafanya kazi pamoja,” amesema.
Mahiga amesema hawa wanaosambaza taarifa hizi kwenye vyombo vya habari au ambao wanazungumza bungeni wanalo lao jambo.
“Tuwe macho inawezekana hata watu wa nje wanaingilia kujaribu kutugombanisha… lakini nachukua nafasi hii tena kwa niaba ya serikali na rais wangu kuwahakikishia watu wa Kenya, serikali ya Kenya, vyombo vya habari hatuingilii uchaguzi wa Kenya,” alisema.