Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 10:47 pm

NEWS: MAHAKIMU WAMETAKIWA KUACHA TABIA YA KUHAIRISHA HAIRISHA KESI

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka Mahakimu wote nchini kusimamia uendeshaji wa mashauri na kuzuia maahirisho ya mara kwa mara ya kesi bila ya sababu za msingi kwa lengo la kuhakikisha kesizinamalizika kwa wakati na kwa haraka Mahakamani.

Prof. Juma amesema hayo jana Septemba 1, 2019 wakati wakikao cha majumuisho mara baada ya kumaliza ziara ya kikazi ya siku tano katikamikoa ya Iringa na Njombe aliyoifanya kwa lengo la kukagua shughuli zaMahakama pamoja na kubainisha kwa wadau changamoto zilizoibuliwa wakati wakikao cha Mahakama ya Rufani kilichomalizika leo mjini Iringa.

Jaji Mkuu amewata Mahakimu kutokubali kuahirisha mashauri kwa muda mrefukwa ajili ya kuandaa maamuzi madogo yanayotokana na pingamizi ambazo nyingihutumiwa vibaya kwa lengo la kuchelewesha mashauri.

“Maafisa wote wa Mahakama ni jukumu lenu pia kuzipa nguvu za kimahakamavifungu vya sheria zinazolinda haki ya Mwananchi aliye mahabusu kwakuhakikisha hakuna mwananchi atashikiliwa bila kufikishwa mahakamani ndani yasiku zilizowekwa na sheria”, alisema.

Alitoa rai kwa Mahakimu kutokuwa wepesi kukubali hoja za waendesha mashitakaza kusema kuwa upelelezi bado unaendelea bila ya kufafanua ni kitu gani katikaupelelezi bado kinatafutwa na ni kwa muda gani.

“Ni umakini wa Mahakama ndiyo utahakikisha kuwa shughuli za upelelezi haziwanyimi wananchi haki yao ya kikatiba ya kutochelewesha haki yao ya kusikilizwa kesi dhidi yao bila sababu za kimsingi,” alisisitiza Jaji Mkuu.

Akizungumzia dhamana, Jaji Mkuu amesema ni wajibu wa Mahakama kutoa dhamana kwa makosa yenye dhamana kwa kuwa Mahakama ni msimamizi wahaki ya kila mtu kuwa huru na kuishi kama mtu huru.

Alivitaja vigezo vya kutumiwa katika kutoa dhamana kuwa ni pamoja na vitambulisho vya Taifa, na vitambulisho vinavyokubalika. Aliongeza kuwa Mahakama pia ziwaruhusu washtakiwa kujidhamini wenyewe pale Hakimu

anapojiridhisha na utambulisho wao kuwa watahudhuria mahakamani. “Mashauri ambayo washtakiwa wamekosa dhamana yasikilizwe mfululizo, kwayale makosa yasiyo na dhamana na yako ndani ya mamlaka ya Mahakama,matumizi ya sheria yatumike ili kuyaondosha”, alisema.

Katika kupunguza msongamano magerezani, Jaji Mkuu amesema Maafisa waMahakama hawana budi kutumia adhabu mbadala kwa makosa madogo madogokwa kuzingatia sheria zilizopo.