- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAHAKAMA ZA KENYA ZAKINZANA KWENYE MAAMUZI JUU YA KARATASI ZA KURA
Nairobi: Tume ya uchaguzi nchini kenya (IEBC) Imeshinda kesi ya Rufaani dhidi ya kesi iliyofunguliwa na Upinzani nchini humo na kutolewa uwamuzi na mahakama kuu, Sasa Mahakama ya Rufaa nchini Kenya imebatilisha uamuzi wa Mahakama Kuu uliokuwa umefuta kandarasi ya kupiga chapa karatasi za kura za urais kufuatia kesi iliyokuwa imewasilishwa na muungano wa upinzani.
Majaji wa mahakama ya rufaa wamesema mahakama kuu ilikosea kwenye kutoa maamuzi, ilipoamua kwamba wananchi walifaa kushirikishwa katika uamuzi wa kutoa kandarasi hiyo ya thamani ya $24m (£18m) kwa kampuni ya Al Ghurair kutoka Dubai.
Tume ya uchaguzi kenya IEBC
Mahakama ya rufaa imesema kuwa si lazima kwa taasisi ya serikali inapoamua kutoa zabuni moja kwa moja kushirikisha wananchi katika kufanya uamuzi au hata kufikia uamuzi wenyewe wa kutumia njia hiyo kutoa kandarasi hiyo.
umoja wa upinzani nchini kenya NASA
mahakama hiyo imesema ni lazima uchaguzi mkuu ufanyike tarehe 8 Agosti na majaji wa Mahakama Kuu walifaa kuzingatia muda uliopo kwa Tume ya Uchaguzi (IEBC) kujiandaa ili kufanikisha uchaguzi huo.