Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 11:25 pm

NEWS: MAHAKAMA YAZUIA KUFANYIKA KWA UCHAGUZI JIMBO LA NASSARI

Dodoma: Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma imezuia kufanyika kwa uchaguzi katika jimbo la Arumeru Mashariki hadi kesi ya maombi madogo ya kufungua kesi ya msingi ya kuomba kutengua uamuzi wa Spika wa kumfutia ubunge wa Jimbo hilo Joshua Nassari itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

Amesema pia wajibu maombi ambao ni Spika na mwanasheria mkuu wa Serikali wamepewa siku saba kupeleka kiapo kinzani cha maombi hayo. “Jaji pia ameagiza kusifanyike uchaguzi wowote (jimboni) hadi hapo maombi hayo yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi,” amesema.

Akizungumza leo Machi 20, 2019 jijini Dodoma naibu msajili wa Mahakama hiyo, Dayness Lyimo amesema kesi ya Mbunge huyo namba 22 ya mwaka 2019 imepangiwa kusikilizwa na Jaji Latifa Mansoor.

Katika kesi hiyo Joshua Nassari anawakilishwa na mawakili watatu ambao ni Hekima Mwasipe, Jonathan Mndeme na Fred Kalonga.

Nassari alivuliwa Ubunge na Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Job Ndugai tarehe 14 machi 2019 kwa madai kuwa mbunge huyo amepoteza sifa za kuwa mbunge baada ya kutohudhuria vikao vitatu vya bunge mfululizo.

Nassari aliongea Jumapili Machi 17, 2019 na waandishi alisema kuwa Tarehe 27 siku ambayo mke wake alijifungua mtoto siku ya pili 28 ndio ilikuwa siku ya kuanza kwa mikutano ya Bunge kwahiyo alitakiwa kuchagua aidha kwenda bungeni kwa ajili ya kuhudhuria vikao au kubaki na kumuuguza mkewe ambaye anadai alikuwa mahututi "nilikuwa na machaguo mawili tu nimwache mke wangu akiwa mahututi niende nikasaini posho bunge au kumuuguza mke wangu." amesema Nassari “Ieleweke kwamba ukiwa Mbunge haiondoi Ubinadamu wa kawaida wala haiondoi majukumu mengine ya kifamilia kama Binadamu mwingine yeyote” ameongeza Nassari

Spika nduagai alimuandikia barua Mwenyekiti wa NEC Jaji Semistocles Kaijage kumtaarifu kuwa jimbo la Arumeru Mashariki linaloongozwa na mbunge huyo liko Wazi kwa sasa hivyo aandae mazingira ya Mchakato wa Uchaguzi

Spika alisema kuwa alichukuwa uwamuzi wa kumfuta ubunge Mbunge huyo Kijana kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 71(1) (c) ibara hiyo inaeleza kuwa mbunge atakoma kuwa mbunge na ataacha kiti chake kama mbunge ikiwa ataacha kuhudhuria mikutani mitatu ya Bungu mfululizo bila kibali cha Spika.