Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 5:35 pm

NEWS; MAHAKAMA YAWAKATALIA DR MASHINJI NA MATIKO KUSAFIRI NJEE YS NCHI

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam nchini imewakatalia viongozi wawil iwa chama kikuu cha upinzani Chadema Dkt Mashinji na Ester Matiko kusafiri nje ya nchini kwa ajili ya kuhudhuria mkutano.

Washtakiwa hao ambao ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko.

Uamuzi wa kuwakatalia viongozi hao umetolewa leo Jumatano Septemba 25, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya kupitia maombi yaliyowasilishwa jana Jumanne na upande wa utetezi wakiomba washtakiwa hao kuruhusiwa kusafiri nje ya nchi.

Hakimu Simba amesema endapo atawaruhusu washtakiwa hao wasafiri nje ya nchi, kesi hiyo itashindwa kuisha kwa wakati.

"Kama washtakiwa hawa nikiwaruhusu wasafiri, wengine wakiomba kusafiri sitaweza kuwakatalia na matokeo yake kesi hii itachukua muda kuisha" amesema Hakimu Simba.

Hakimu Simba ametoa uamuzi huo, wakati kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa Chadema walipofikishwa mahakama hapo kwa ajili ya washtakiwa hao kuanza kujitetea, baada ya kukutwa na kesi ya kujibu.



Hakimu huyo ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 7, 2019 itakaposikilizwa kwa siku tano mfululizo yaani Oktoba 7, 8, 9, 10 na 11, 2019.

Mbali na Matiko na Dk Mashinji wengine ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Pia wabunge wa Chadema, Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini), John Heche (Tarime Vijijini), Halima Mdee (Kawe), Ester Bulaya (Bunda Mjini), John Mnyika wa Kibamba pamoja na Naibu Katibu Mkuu- Zanzibar, Salum Mwalimu.

Washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13 yakiwemo ya uchochezi.