Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 5:31 am

NEWS: MAHAKAMA YAWAITA KWENYE KESI ZITTO NA SPIKA NDUGAI

Dar es Salaam: Kesi ya Kikatiba namba 01/2019 iliyofunguliwa Mahakama Kuu, Masjala Kuu Dar es salaam na mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe dhidi ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kuhusu kinga ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwa mujibu wa Katiba ya Nchi na Mamlaka ya Bunge inawaita na kuwahoji watu mbalimbali,leo Januari 31, 2019.

Mahakama hiyo imetoa wito kwa mdai- Zitto na mdaiwa-Spika ikiwataka kufika mahakamani leo kesi hiyo itakapotajwa kwa mara ya kwanza.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Firmin Matogolo, Dk Benhajj Masoud na Elinaza Luvanda.

Katika kesi hiyo, Zitto ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo anaiomba Mahakama Kuu itoe tafsiri ya kinga ya CAG iliyopo kikatiba na tafsiri ya Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge katika kushtaki watu wanaosemekana kulidharau Bunge.

Zitto alifungua kesi hiyo baada ya Spika kupitia kwenye vyombo vya habari na baadaye kumwandikia barua CAG, Profesa Mussa Assad akimtaka afike mbele ya kamati ya Bunge kuhojiwa kutokana na kauli aliyoitoa akiwa Marekani kuwa Bunge ni dhaifu.

Profesa Assad alitoa kauli hiyo kama maoni yake wakati akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya Umoja wa Mataifa, kulingana namna taarifa zake za ukaguzi zinavyofanyiwa kazi.

Kesi hiyo ilisajiliwa Januari 21 baada ya kukwama kwa siku saba kutokana na mvutano uliokuwapo baina ya upande wa mdai na Mahakama kutokana na kasoro zilizoainishwa