- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAHAKAMA YAWAFUTIA KESI KAMISHNA WA TRA NA MISS TANZANIA
Dar es Salaam. Leo Ijumaa 11, 2019 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewafutia mashtaka aliyekuwa Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Harry Kitillya na mwenzake wawili ambao ni maofisa wa benki ya Stanbic, Shose Sinare na Sioi Solomon.
Uwamuzi wa kuwafutia mshitaka hayo umefikiwa leo na Hakimu mkazi Salum Ally baada ya mkurungezi wa mashtaka DPP kuwa hana niya ya kuendelea na shauri hilo
Washtakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na mashtaka nane yakiwemo ya kutakatisha fedha. Wamefutiwa kesi hiyo chini ya kifungu namba 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai (CPA), sura ya 20, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002
Wakili Mkuu wa Serikali, Hashimu Ngole akisaidia na wenzake Pendo Mangole na Patrick Mwida, amedai mahakamani hapo kuwa DPP hana nia ya kuendelea na shauri hilo dhidi ya washtakiwa hao. "Taarifa hii ya kutokuendelea na shauri hili mbele ya mahakama yako, imeletwa chini kifungu namba 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), sura ya 20, iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002," amesema Ngole. Baada ya maelezo hayo, Hakimu Ally alisema kutokana na maombi hayo, mahakama hiyo imeifuta kesi hiyo.
washtakiwa hao baada ya kufutiwa kesi hiyo, wamekamatwa tena na kuwekwa chini ya Ulinzi na Kurudishwa mahabusu