- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAHAKAMA YATOA HATI YA KUKAMATWA RAIS JACOB ZUMA
Mahakama ya mjini Pietermaritzburg nchini Afrika Kusini ambayo ni ya juu kabisa nchini humo , imetoa hati ya kukamatwa kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma baada ya kushindwa kufika katika mahakama hiyo kukabiliana na mashtaka dhidi yake kuhusu rushwa na Ubadhirifu wa mali.
Hati hiyo itafanya kazi ikiwa atashindwa kuhudhuria kesi yake itakayoanza mwezi Mei. Bwana Zuma anakabiliwa na makosa 16 ya kughushi, rushwa , ulaghai na utakatishaji fedha ukihusisha biashara ya silaha ya thamani ya mabilioni ya dola iliyofanywa tangu miaka ya 1990.
Rais huyo wa zamani amefanikiwa kukwepa shutuma za rushwa dhidi yake kwa zaidi ya miaka 10. Lakini leo, sheria haikuwa upande wake.
Hati ya kukamatwa kwake imetolewa baada ya kushindwa kufika mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi yake. Jopo la wanasheria wake waliwasilisha nyaraka wakisema kuwa mteja wao alikuwa mgonjwa na amekuwa akipatiwa matibabu nje ya Afrika Kusini tangu mwezi uliopita.
Jaji Dhaya Pillay alihoji maelezo yaliyo kwenye nyaraka za matibabu za Zuma zilizowasilishwa na mawakili wake mahakamani. Lakini rais huyo wa zamani atakamatwa ikiwa atashindwa kufika mahakamani tarehe 6 mwezi Mei kesi yake itakapoanza rasmi.
Bwana Zuma anakabiliwa na mashtaka kadha wa kadha ya rushwa ikihusisha malipo 783 yenye utata anayodaiwa kupokea kutoka kwa aliyekuwa mshauri wake wa masuala ya fedha Schabir Shaik.
Madai hayo pia yamerejelea mkataba wa silaha uliofanyika miaka ya 1990 na kampuni moja ya masuala ya ulinzi ya nchini Ufaransa.