- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAHAKAMA YATAKA KUKAMILIKA KWA UPELELEZI KESI YA WEMA
Dar es Salaam: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewataka upande wamashtaka(Jamhuri) kuhakikisha upelelezi wa kesi inayomkabili Miss Tanzania wa 2006, Wema Abraham Sepetu unakamilika kwa wakati ili kesi iweze kuendelea, huku akisema kesi hiyo inamuda mrefu tangu ifunguliwe.
"Nataka upande wa mashtaka mkamilishe kwa wakati upelelezi ili kesi iweze kuendelea kwa sababu ni kesi ya muda mrefu tangu ifunguliwe mahakamani hapa Novemba mwaka jana na hadi sasa upelelezi bado,β amehoji Kasonde. Awali, wakili wa Serikali, Mosia Kaima amedai kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wake bado haujakamilika. Aliiomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi wa shauri hilo utakuwa umekamilika ama la.
Nae wakili wa Wema, Ruben Simwanza aliieleza mahakama kuwa kesi hiyo imeshatajwa mara nne mahakamani hapo huku upelelezi wake ukiwa bado. "Naomba upande wa mashtaka ujitahidi kukamilisha upelelezi kwa wakati kwa sababu shauri hili limeshatajwa kwa mara ya nne sasa, bila upelelezi wake kukamilika," amedai Wakili wa Utetezi.
Hakimu Kasonde baada ya kusikiliza hoja za pande zote ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 13, 2019 itakapotajwa tena na kuwataka upande wa mashtaka kuhakikisha wanakamilisha upelelezi wao kwa wakati.
Wema anakabiliwa na shtaka moja la kuchapisha video ya ngono na kusambaza katika mitandao ya kijamii. Uamuzi huo umetolewa leo na Hakimu Mkazi, Maira Kasonde, baada ya upande wa mashtaka kudai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.
Wema alifikishwa kwa mara ya kwanza Kisutu, Novemba Mosi, 2018 kujibu shtaka hilo. Hata hivyo baada ya kusomewa shtaka hilo na kukana, alitakiwa kutoweka video zinazohusiana na ngono wala maneno yoyote yenye mwelekeo huo katika mtandao wake.