- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAHAKAMA YATAIFISHA BILIONI 16 ZA UPATU
MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi (mahakam ya Mafisadi) imetaifisha zaidi ya Sh bilioni 16.7 zilizokuwa zikimilikiwa na Kampuni ya IMS Marketing Tanzania Limited iliyojihusisha na biashara haramu ya upatu na kuwa mali ya serikali.
Aidha, mahakama hiyo imekataa ombi la Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) alilokuwa akiiomba mahakama itoe amri ya kuamrisha Benki ya Afrika (BOA), kulipa riba ya kipindi chote walichohifadhi fedha hizo ambazo zinamilikiwa na raia wawili wakigeni, Manon Hubenthal, mkazi wa Greven nchini Ujerumani na Frank Riketits, Mkazi wa Blackwats Uingereza.
wote wakiwa Wakurugenzi na Wanahisa wa kampuni hiyo.
Katika uamuzi uliosomwa mahakamani hapo leo aprili 3,2020 na Jaji Elinaza Luvanda amesema DPP aliwasilisha maombi ya kutaka mahakama itaifishe mali ambazo ni USD 1,351,597.79 na Euroq 5,377,306.56, zote mbili zikiwa kwa jina la IMS Marketing Tanzania Limited zilizofunguliwa katika benki ya BOA.
Amesema mali hizo zilitokana na biashara ya upatu licha ya kwamba kampuni hiyo ilisajiliwa kwa shughuli za masoko.
Akisoma uamuzi huo Jaji Luvanda amesema awali DPP aliwasilisha maombi yaliyoungwa mkono na hati za kiapo za Wakili wa Serikali, Estazia Wilson na Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Fadhili, wakielezea jinsi washitakiwa hao walivyohusika katika kutenda uhalifu wa kuendesha mpango wa upatu na kutakatisha fedha.
"Wadaiwa waliitwa kupitia matangazo mbalimbali lakini hawakuthubutu kuwasilisha kiapo kinzani na hata kesi ilipofunguliwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu zilitolewa hati za kuwakamata lakini walikuwa mafichoni hivyo katika hali hii wajibu maombi hawakukana hati ya kiapo hivyo waleta maombi wamethibitisha maombi yao na fedha zinataifishwa kuwa mali ya serikali," amesema Jaji Luvanda.
Hata hivyo, Jaji Luvanda amesema analikataa ombi la DPP la kutaka mahakama itoe amri ya kuamrisha BOA kulipa riba ya kipindi chote walichohifadhi fedha hizo kwa sababu kiasi cha riba hakikuelezwa kwenye hati ya kiapo benki ya BOA sio wadaawa katika maombi hayo na hawakuitwa kujitetea hivyo, akitoa amri dhidi yao kwa maoni yake ni kukiuka haki yao ya kusikilizwaa.
Pia ameongeza kuwa haikuelezwa ni kwa namna gani benki hiyo ingenufaika na fedha hizo walizohifadhi hivyo, alishauri waleta maombi kutafuta njia nyingine ya kuwasilisha ombi kuhusu riba.
Awali DPP Biswalo Mganga akisaidiana na Wakili Mkuu wa Serikali, Shadrack Kimaro na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Christopher Msigwa waliomba amri ya kutaifisha fedha hizo ili kuzuia wahalifu kufaidika na makosa ya jinai waliyotenda huku pia akiiomba Mahakama kuiagiza Benki ya BOA Limited kulipa riba kwa kukaa na kiasi hicho kikubwa cha fedha tangu Januari 19, 2018, wakati wakijua fedha hizo sio halali