- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAHAKAMA YAPATILISHA WAKURUGENZI KUSIMAMIA UCHAGUZI NCHINI
Dar es salaam: Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam imebatilisha vifungu vya sheria vilivyokuwa vikiwapa mamlaka Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kusimamia Chaguzi.(Uchaguzi wa Urais, Ubunge, na Udiwani)
Hukumu ya Kesi hiyo namba 6, ya mwaka 2018 imetolewa leo May 10, 2019 ambayo kesi hiyo ilifunguliwa na mtoto wa Mbunge wa Zamani wa chadema Chacha Wangwe anayeitwa Bobu Wangwe dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) mwaka jana.
Aidha Katika kesi hiyo, Wangwe aliyekuwa akiwakilishwa na Wakili Msomi ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Rais wa Zanzibar Amani Karume , Fatuma Karume, anapinga Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa kuwa wasimamizi wa uchaguzi kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini(NEC)
Anadai kuwa hiyo ni kinyume cha Ibara ya 74 (14 ) ya Katiba ya Nchi ambayo inapiga marufuku kwa mtu yeyote anayehusika na uchaguzi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa na kwamba ana haki ya kupiga kura tu
Pia Wangwe katika kesi hiyo amedai kuwa wakurugenzi hao wanaosimamia chaguzi nchini ni wateule wa Rais ambaye pia kimsingi ni mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM).