Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 10:42 am

NEWS: MAHAKAMA YAMUONYA VIKALI MSANII WEMASTU

Dar es Salaam: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam nchini Tanzania imemuonya vikali msanii wa Filamu nchini na Mlimbwende (2006), Wema Sepetu(30), kukiuka masharti ya dhamana yake, vinginevyo haitasita kufutilia mbali dhamana yake hatua ambayo itampelekea kukaa gerezani mpaka mwisho wa huku ya kesi hiyo.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatayu, Juni 24, 2019 na Hakimu Mwandamizi wa mahakama hiyo, Maira Kasonde wakati akitoa uamuzi kuhusiana na mshtakiwa kukiuka masharti ya dhamana.

Kama utakumbuka Juni 17, 2019 Mahakama hiyo iliamuru mshtakiwa huyo kupelekwa rumande hadi leo Jumatatu, ili iweze kutoa uamuzi baada ya mshtakiwa huyo kujisalimisha mahakamani hapo.

Wema alijisalimisha mahakamani hapo Juni 17, 2019 baada ya Mahakama hiyo kutoa hati ya kumkamata mshtakiwa huyo kutokana na kushindwa kufika mahakamani bila kutoa taarifa.

Mahakama ya Kisutu, ilitoa hati ya kumkamata Wema, Juni 11, 2019 baada ya mshtakiwa huyo kuruka dhamana.