- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAHAKAMA YAMUACHILIA HURU MBUNGE CECIL MWAMBE
Mahakama ya Mkoa wa Mtwara, imemwachia huru aliyekuwa Mbunge wa Ndanda (Chadema), Cecil Mwambe katika kesi ya uchochezi namba 263 ya mwaka 2017 iliyokuwa inamkabili.
Katika kesi ya msingi Mwambe alishitakiwa kwa makosa mawili, kosa la kwanza, kutoa kauli za uchochezi alizotoa katika Kata Reli, wilaya Masasi, huku kosa la pili ni kufanya njama ya kutaka kutenda ovu.
Hakimu Kabate R. ametoa uamuzi huo wa kumwachia huru Mwambe leo Aprili 30, 2020 baada ya upande wa mashataka kushindwa kuthibitisha pasipo shaka kuwa mtuhumiwa alitenda makosa hayo, ambayo pia hayakuleta athari yoyote kwa jamii husika.
Mwambe alifunguliwa kesi hiyo akiwa Mbunge wa Ndanda kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) lakini alijivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).